Skip to main content

Sudan yapokea dozi milioni 2 kukabiliana na mlipuko wa Surua

Sudan yapokea dozi milioni 2 kukabiliana na mlipuko wa Surua

Mashirika ya Umoja wa mataifa ikiwemo lile la afya duniani WHO na lile la kuhudumia watoto UNICEF na wizara ya afya nchini Sudan yamepokea dozi milioni mbili za chanjo dhidi ya Surua kufuatia mlipuko wa ugonjwa huo katika majimbo 23 katika miezi ya hivi karibuni.

Idadi hiyo ya chanjo ni  sehemu ya ombi la dozi milioni 9.6 lililokuwa limewasilishwa ili kuwezesha kampeni ya kutoa chanjo katika maeneo yalioathirika na Surua.

Katika juhudi za kukabiliana na mlipuko huo WHO kwa kushirikiana na wizara ya afya nchini Sudan ilipendekeza kutengwa kwa dola milioni 3.9 kutoka mfuko wa Surua na Rubella (MRI) ili kugharamia ununuzi wa chanjo na vifaa na vifaa tiba ili kuwezesha kudhibiti na kukabiliana na surua .