Maelfu wanaswa kambini Yarmouk, Syria: UM

8 Aprili 2015

Umoja wa Mataifa umelezea wasiwasi wake kuhusu hatma ya maelfu ya raia walionaswa katika kambi ya Yarmouk, mjini Damascus nchini Syria.

Kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric, wapigananaji wa kundi la kigaidi linalotaka dola la kiisalamu wenye msimamo mkali, ISIL, lilivamia kambi hiyo juma lililopita na kuwalazimisha mamia ya watu kukimbia huku maelfu ya wakimbizi wa Palestina wakiendelea kusalia katika sintofahamu wakati mapigano kati ya vikosi vyenye silaha yakiendela katika maeneo ya kambi.

Bwana Dujarric amewaambia waandishi wa habari mjini New York kuwa hali katika eneo hilo bado ni tete, mapigano yakiendelea huku kukiwa na taarifa ambazo hazijathibitishwa zikisema kuwa kuna mashambulio ya angani yanayolenga raia.

Amesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Palestina UNRWA raia 18,000 hao wanaendelea kupata dhiki kutokana na uhasama unaeondelea ambapo wanaume, wanawake,na watoto kutoka Palestian na Syria wamenaswa kambini Yarmouk huku ikitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano ili kufikisha misaada ya kibinadmau kwa wahitaji ikiwamo kuondolewa salam aeneo hilo hatari

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter