Skip to main content

IAEA yakaribisha juhudi za Misri kutumia nyukilia kwa faida

IAEA yakaribisha juhudi za Misri kutumia nyukilia kwa faida

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nishati ya atomiki duniani IAEA, Yukya Amano amepongeza umuhimu wa Misri kuonyesha utashi wa  kutumia utaalamu wake katika sayansi ya nyukilia na teknolijia na nchi nyingine za ukanda huo.

Akizungumza baada ya kukutana na waziri wa mambo ya kigeni wa Misri hapo jana Bwana Amano aligusia faida za matumizi chanya ya  sayansi ya nyukilia na teknolojia kwa wanadmau na afya za wanyama, uzalishaji wa chakula na matumizi ya rasilimali za maji pamoja na uzalishaji wa umeme.

Amesema Misri ni mshirika muhimu kwa IAEA na kwamba shirika lake limefanya kazi nchini humo ikiwamo uzalishaji wa kemikali za madawa, vyanzo vya maji na usalama wa chakula.