Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtalaam wa UM alaani ubaguzi dhidi ya Waroma

Mtalaam wa UM alaani ubaguzi dhidi ya Waroma

Watu we kabila la Waroma barani Ulaya wanazidi kukumbwa na ubaguzi na ukatili, amesema Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu makundi ya walio wachache Bi Rita Izsak, leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya Waroma.

(SAUTI RITA)

“ Kinachonipa wasiwasi sana ni kuongezeka kwa idadi ya watu wenye msimamo mkali kote Ulaya. Wamewafanya watu wasiwe tena na huruma. Watu wengi zaidi wanaamini kwamba Waroma ni watu wa chini bila maana, wahalifu, na mara nyingi, viongozi wa kisiasa na jamii wamezidi kuwa kimya.”

Mtalaam huyu amezisihi viongozi kuwajibika kwa kupambana na ubaguzi na unyanyapaa dhidi ya Waroma kwa kuheshimu haki za walio wachache, demokrasia na utawala bora.

Aidha ametoa wito wa kuimarisha uwakilishaji wa kundi hilo katika asasi za kuchukua maamuzi katika ngazi ya kijamii, kitaifa na kimataifa.