Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Yemen hakufikiki kwa sasa: UNICEF

Yemen hakufikiki kwa sasa: UNICEF

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Yemen amesema ni vigumu kufikisha misaada ya kibinadamu katika ardhi ya nchi hiyo inayoshuhudia mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi.

UNICEF ilipanga kufikisha kwa njia ya anga tani 16 za misaada ya kitabibu katika mji mkuu San’aa Alhamisi juma hili lakini mwakilishi wake Julien Harneis anasema usalama hautoshi hilo kufanyika kutokana na mazingira hatarishi yanayowakumba raia wa Yemen kwa muda mrefu ikiwamo unyafuzi.

Katijka mahojinao na redio ya Umoja wa Mataifa amesema kufuatia kuzorota kwa usalama hakuana uhakika kuwa wahitaji wa misaada watafikiwa.

(SAUTI JULIEN)

"Tutaweza kusafirisha misaada Kaskazini na Kati mwa nchi pekee, lakini ni vigumu kufika katika maeneo kama vila Aden. Kuna mashirika menginje yanafanya kazi hapo kwahiyo nafikiri tunaweza kutumia njia hiyo. Hata hivyo ni hatari kuzunguka katika nchi."