Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa UNCTAD utamulika Biashara ya bidhaa

Mkutano wa UNCTAD utamulika Biashara ya bidhaa

Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD itafanya kongamano la siku mbili kuhusu bidhaa za kimataifa mjini Geneva wiki ijayo. Mkutano huo wa sita  wenye kauli mbiu “Biashara ya bidhaa:changamoto na fursa utaanza Aprili 13 hadi 14.Taarifa zaidi na Grace Kaneiya

(Taarifa ya Grace)

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva kuhusu mkutano huo Mkuu wa kitengo cha bidhaa Samuel Gayi mchumi katika UNCTAD amesema kwamba mwaka jana kulishuhudiwa kupungua kwa bei za bidhaa na kongamano hili litakuwa ni fursa ya kuangalia ikiwemo matokeo yake kwa nchi zinazozalisha bidhaa na wadau katika mzunguko wa kuongeza dhamana.

Kuhusu nchi zinazoendelea Bwana Gayi amesema kwamba mkutano utaangazia sera zilizopo kwa ajili ya fursa za biashara za malighafi

(Clip ya Gayi)

Nchi ambazo zinazalisha malighafi zinapaswa kuwa na vigezo vya juu kuhusu matumizi ya udhibiti wa biashara ya nje kwa sababu inaathiri uwasilishaji kwa wale wanaotumia malighafi.”