Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabomu yadondoka na kuuwa 14 Darfur: UNAMID

Mabomu yadondoka na kuuwa 14 Darfur: UNAMID

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika UNAMID jimboni Darfur nchini Sudan umesema mabomu 10 yaliyodondoka huko Ruata yamesababaisha vifo vya watu 14 na kujeruhi wengine 18 April mosi mwaka huu.

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York leo msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujjaric amesema kikosi maalum cha doria kutoka UNAMID kimefika eneo hilo na kushuhudia mabomu mengine 5 yaliyodondoka karibu na kikosi hicho.

Bwana Dujjaric amesema vitendo hivyo havikubaliki

(SAUTI DUJJARIC)

"Ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaalani ulipuaji wa mabomu kama huo unaosababisha vifo, uharibifu na ukosefu wa makazi kwa watu."

Katika hatua nyingine amesema takribani wakimbizi wa ndani  4500 hatimaye wamepata malazi katika makao ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudani Kusini, UNMISS yaliyoko Malakal na jimbo la Upper Nile na kufanya idadi ya wakimbizi wa ndani wanaohifadhiwa katika vituo vya UNMISS kufikia zaidi ya 150000 nchi nzima .