Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa Rwanda asema ni lazima kupambana na fikra za mauaji ya kimbari

Mwakilishi wa Rwanda asema ni lazima kupambana na fikra za mauaji ya kimbari

Leo ikiwa ni miaka 21 baada ya kuanza kwa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, Umoja wa Mataifa pamoja na Ujumbe wa Kudumu wa Rwanda kwenye Umoja huo wameandaa kumbukizi maalum jijini New York, kwa ajili ya kukumbuka mateso dhidi ya watutsi na baadhi ya wahutu walioyoyapitia nchini Rwanda mwaka 1994.

Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Rwanda kwenye Umoja wa Mataifa, Jeanne d’Arc Byaje, ameeleza kwamba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Ban Ki-moon, Rais wa Baraza Kuu, na mabalozi Samantha Powers wa Marekani na Antonio Tete wa Muungano wa Afrika watahudhuria hafla hiyo, ikihutubiwa pia na manusura mmoja. Bi Byaje amesema ni muhimu kukumbuka mauaji hayo ili watu wasisahau na vitendo kama hivyo visitokee tena, pamoja na kupambana na fikra za mauaji ya kimbari, ikiwa ni maudhui ya mwaka huu. Akihojiwa na Priscilla Lecomte kutoka Idhaa hii, Bi Byaje ameanza kwa kueeleza kwa nini ni vigumu kwa manusura kukumbushwa mateso waliyoyapitia.