Kutoka shambani hadi mezani, usalama ukoje?

7 Aprili 2015

Katika kuangazia siku ya afya duniani hii leo, Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amerejela umuhimu wa kusimamia usalama wa chakula kwa kuwa kinyume na hapo, vyakula vyenye vijidudu na kemikali zisizotakiwa husababisha zaidi ya aina 200 za magonjwa.

Ban katika ujumbe wake ametaja magonjwa hayo kuwa ni pamoja na kuhara, kipindupindu hadi saratani akisema kuwa zama za sasa vitisho vipya vya usalama wa chakula vinaibuka kutokana na mfumo mzima wa uzalishaji, usindikaji, usafirishaji na usambazaji wa vyakula.

Amesema ni nadra sana vyakula visivyo salama huripotiwa na hivyo tatizo linaweza kuwa kubwa kuliko inavyotambulika na hivyo ametoa wito kwa serikali kuimarisha usimamizi wa usalama wa chakula.

Dkt. Kazuaki Miyagishima ni Mkurugenzi wa Usalama wa chakula wa shirika la afya duniani, WHO.

(Sauti ya Dkt. Miyagishima)

Chakula kinaweza kupata uambukizi wa virusi au kemikali na hivyo kusababisha aina zaidi ya 200 za magonjwa. Sekta kama vile kilimo, uvuvi, viwanda, utalii, biashara na utalii zinapaswa kushirikiana ili kukabiliana na tatizo hili.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter