Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya vifo vya watoto yaongezeka Yemen.

Idadi ya vifo vya watoto yaongezeka Yemen.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF limeonya kuhusu kuzorota zaidi kwa hali ya kibinadamu nchini Yemen, likisema inaathiri zaidi watoto. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

UNICEF imesema takribani watoto 74 wameuawa na wengine 44 wamelemazwa tangu kuongezeka kwa mapigano kaskazini na kusini mwa nchini, mwisho wa mwezi uliopita, wakati zaidi ya watu 100,000 wamelazimika kuhama makwao.

Christophe Boulierac, msemaji wa UNICEF, ameeleza hayo alipozungumza na waandishi wa habari mjini Geneva:

“ Mzozo unazidisha hali ambayo tayari ni ya hatari kwa watoto. Maeneo mengi ya nchi hii ambayo ni miongoni mwa nchi maskini zaidi za ukanda huu, tayari yameathirika na ukosefu wa usalama wa chakula na utapiamlo wa kupindukia ambao uliotapakaa kwa watoto.”

Ametoa wito kwa pande zote za mzozo kuheshimu haki za watoto na kulinda hali yao ya kibinadamu akiongeza kwamba tayari UNICEF inatoa huduma za maji safi na afya, na vyakula kwa ajili ya watoto wadogo.