Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mauaji ya kimbari ya Rwanda yakumbukwa leo na Umoja wa Mataifa

Mauaji ya kimbari ya Rwanda yakumbukwa leo na Umoja wa Mataifa

Leo ikiwa ni siku ya kukumbuka mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda miaka 21 iliyopita, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ni wakati mwafaka kukumbuka watu 800,000, hasa watutsi, waliouawa. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla)

Bwana Ban ameongeza kwamba ni fursa kukumbuka pia makosa yaliyofanywa zamani na kuhakikisha hayatokei tena, na kuchukua hatua mapema kabla mauaji hayajaanza.

Wakati kumbukizi maalum itafanyika leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Balozi Jeanne d’Arc Byaje, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Rwanda kwenye Umoja wa Mataifa, ameiambia Idhaa hii kwanini ni muhimu kuendelea kukumbuka mauaji hayo.

(Sauti ya Balozi Byaje-1)

Akaenda mbali zaidi kuhusu mustakhbali wa usalama wa Rwanda kwenye ukanda wa Maziwa Makuu ..

(Sauti ya Balozi Byaje-2)