Nishati ya jotoardhi ni fursa ya usalama wa chakula kwa nchi zinazoendelea:FAO

7 Aprili 2015

Ripoti mpya ya shirika la chakula na kilimo duniani, FAO imesema nishati ya jotoardhi ni fursa inayoibuka kwa nchi zinazoendelea kwa kuwa gharama yake ni nafuu na inawezesha uendelevu kwenye uzalishaji na usindikaji wa vyakula.

FAO inasema licha ya uwepo wa vyakula vyingi katika nchi hizo, bado kiasi kikubwa hupotea baada ya mavuno kutokana na ukosefu wa nishati nafuu ya kuvisindika.

Ukaushaji wa vyakula unaweza kuongeza muda wa matumizi wa vyakula na virutubisho vyake kama vile samaki, maziwa na mboga za majani, imesema FAO ikitanabaisha kuwa vinaweza kuhifadhiwa na kutumiwa kwa mwaka mzima hata wakati wa ukame.

Divine Njie Naibu Mkurugenzi wa FAO kitengo kinachohusika na viwanda vya mazao ya kilimo amesema ni muhimu serikali zikawekeza katika sekta hii akielezea kile ambacho ripoti imeweka bayana.

(Sauti ya Divine)

"Mfano Kenya ambako serikali imechukua hatua za kisera na mfumo wa usaidizi kwa taasisi unaohitajika , na pia sio tu inakupatia mifano ya nini nchi nyingine zimefanya bali pia fursa mbali mbali ambazo zimechukua katika mzunguko mzima wa uongezaji wa thamani.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter