Hisia mchangayiko utokomezaji silaha za nyuklia: Kane

6 Aprili 2015

Mkuu wa masuala ya kutokomeza silaha wa Umoja wa Mataifa Angela Kane amesihi nchi wanachama wa Umoja huo kusaka msimamo wa pamoja juu ya utokomezaji silaha.

Akihutubia wajumbe kwenye ufunguzi wa mkutano wa Kamisheni ya utokomezaji silaha ya Umoja wa Mataifa UNDC jijini New York siku ya Jumatatu Bi. kane amesema msimamo wa pamoja ni muhimu wakati huu ambapo kuna ongezeko la tishio duniani la matumizi ya silaha za nyuklia na nyinginezo zinazotishia uhai wa binadamu.

Ameonya kuwa jitihada za kupunguza mzunguko wa silaha duniani zimekumbwa na mkwamo na matumaini ya kutokomeza silaha za nyuklia yana walakini.

Amesema hajawahi kushuhudia mgawanyiko mkubwa kati ya wenye nyuklia na wasio na nyuklia. Mgawanyiko huu kuwa kikwazo dhahiri kwa jitihada za kutokomeza uenezaji wa nyuklia. Akiongeza kwamba ni lazima utokomezwe.

Hata hivyo amesema katika wingu la giza lililotanda kuna matumaini ya dhati ikiwemo kuondolewa kabisa kwa silaha za kemikali nchini Syria na kuanza kutekelezwa kwa mkataba wa kimataifa wa biashara ya silaha, ATT.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter