Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yalaani mauaji ya wauguzi Yemen

WHO yalaani mauaji ya wauguzi Yemen

Shirika la afya duniani WHO limelaani vifo vya wahudumu wa afya na uharibifu wa vituo vya afya nchini Yemen ikiwa ni matokeo ya mapigano yanavyoendelea nchini humo.

Taarifa hiyo inafuatia mashambulizi dhidi ya magari ya wagonjwa yaliyotokea hivi karibuni ambapo wafanyakazi watatu wa kujitolea wameuawa huku pia mlinzi mmoja na wauguzi wawili wakiuwawa kwenye shambulizi dhidi ya kambi la wakimbizi la Al-Mazraq.

Aidha WHO imeeleza wasiwasi wake kuhusu hatari wanazokabiliana nazo wahudumu wa afya nchini Yemen, mapigano yakiendelea nchini humo.

WHO imeongeza kwamba vituo vya afya na magari ya wagonjwa hazipaswi kulengwa na mapigano au kutumiwa kwa ajili ya kupigana, ikizisihi pande zote kutunza wahudumu wa afya na hospitali.