Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Darwish ndiye mshindi wa tuzo ya UNESCO ya Guillermo Cano

Darwish ndiye mshindi wa tuzo ya UNESCO ya Guillermo Cano

Mshindi wa tuzo ya uhuru wa kujieleza ya Shirika la elimu na utamaduni UNESCO ya Guillermo Cano ni mwandishi wa habari na mtetezi wa haki za binadamu Marzen Darwish ambaye kwa sasa anashikiliwa kizuizini.

Tuzo hiyo itatolewa wakati wa siku ya uhuru wa kujieleza Mei 3.  Bwana Darwish amependekezwa kwa kazi kubwa aliyofanywa nchini Syria kwa zaidi ya miaka kumi na kwa kujitolea akikabiliwa na mateso na kufungwa kwa kila mara na kuteswa.

Darwish, ambaye ni wakili na mtetezi wa haki za kujieleza, ni rais wa kituo cha vyombo na uhuru wa kujieleza Syria (CMFE) kilichoanzishwa mwaka 2004 na mmoja wa waanzilishi wa gazeti la Voice na blogi ya Syriaview.net kituo cha habari kilichopigwa marufuku  na mamlaka za Syria. Darwish  alianzisha klabu cha vyombo vya habari yaani Media Club,  jarida la kwanza Syria kwa ajili ya masuala ya upashanaji.

Darwish alikuwa ameshikiliwa kuanzia Februari 2012 alipokamatwa na wafanyakazi wengine akiwemo Hani Al-Zitani na Hussein Ghareer.