Skip to main content

Bei ya vyakula yazidi kushuka: FAO

Bei ya vyakula yazidi kushuka: FAO

Shirika la chakula na kilimo FAO limesema bei ya bidhaa imeendelea kushuka kwa asilimia 1.5 mwezi Machi ikilinganishwa na mwezi Februari na pia ikiwa alama 18.7 ikilinganishwa na mwaka jana.

Kwa mujibu wa FAO kushuka kwa ghafla kwa bei ya sukari ambayo imefikia kiwango cha chini ya zaidi tangu Februari 2009  pamoja na kushuka hima kwa mafuta, nafaka na nyama ambayo ni tofauti na kupanda kwa bei za maziwa vimechangia kuwa na anguko la bidhaa kwa alama 173.8 kwa mwezi Machi.

Shirika  hilo la chakula na kilimo linasema bei za vyakula kwa ujulma zimekuwa zikishuka tangu April mwaka 2014.