Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA yatoa wito wa dharura kwa ulinzi wa raia Yarmouk

UNRWA yatoa wito wa dharura kwa ulinzi wa raia Yarmouk

Shirika la Kuwasaidia Wakimbizi wa Palestina, UNRWA, limetoa wito kwa pande zote zenye silaha kukomesha mapigano ambayo yanawaweka raia hatarini na kuondoka mara moja katika maeneo yanayokaliwa na raia.Taarifa kamili na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

UNRWA imezitaka pande zote zijizuie na kutimiza wajibu wao chini ya sheria ya kimataifa na kuwalinda raia.

Aidha, shirika hilo limezitaka pande kinzani ziwezeshe wahudumu wa kibinadamu kuwafikia raia na kuweka mazingira yanayoruhusu kufikisha misaada ya kibinadamu na kuwezesha raia kuhamishwa kutoka palipo hatari.

UNRWA imewzitaka pia nchi nyingine zitumie mamlaka na ushawishi zilizo nao ili kukomesha mapigano Yarmouk kwa ajili ya uhai wa raia na kumaliza taabu kwa wanadamu.

Sami Mshasha ni msemaji wa UNRWA..

(Sauti ya Sami)