Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICRC kupeleka misaada ya dharura Yemen

ICRC kupeleka misaada ya dharura Yemen

Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu, ICRC, limesema linajiandaa kupeleka misaada ya dharura kwa ndege katika mji mkuu wa Yemen, Sana’a.

Katika taarifa, shirika hilo imesema kuwa limepewa idhini ya kuwezesha ndege zake za kubeba raia na vifaa tiba kutua nchini Yemen, ambayo limesema inakumbwa na hali ya dharura ya kibinadamu.

Mapigano yameripotiwa kuongezeka katika bandari ya kusini ya Aden, majeshi ya serikali yakikabiliana na waasi wa Houthi.

Takriban watu 500 wamuawa katika kipindi cha wiki mbili zilizopita nchini Yemen.

ICRC inapeleka ndege ya mizigo ilosheheni vifaa muhimu, pamoja na ndege ndogo ya abiria ikiwa na wafanyakazi wa misaada

Wapiganajai wanane kutoka kundi la waasi wa Huthi waliuwawa katika shambulio la angani katika makazi ya kusini mwa mji wa Saadah eneo ambalo ni ngome ya kundi la waislamu liitwalo Shi’ite lililosambaa kutoka milimani ili kuuteka mji wa Sanaa miezi sita iliyopita