Skip to main content

Tuko mbali sana na suluhu kati ya Israel na Palestina asema mjumbe wa UM

Tuko mbali sana na suluhu kati ya Israel na Palestina asema mjumbe wa UM

Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu utaratibu wa amani Mashariki ya Kati, Robert Serry, amesema kwamba bado safari ndefu kuhusu suluhu ya mataifa mawili kati ya Palestina na Israel.

Amesema hayo akihojiwa na Redio ya Umoja wa Mataifa wakati wa kuhitimisha miaka saba kwenye Ofisi ya Utaratibu wa amani Mashariki ya Kati, UNSCO.

Ameongeza kwamba waisraeli 500,000 wamehamia katika maeneo ya Palestina kwa kipindi cha miaka sita na hiyo inahatarisha zaidi matumaini ya amani.

Aidha ameelezea wasiwasi wake juu ya hali ya Gaza, akisikitishwa na ukosefu wa ufadhili kwa ukarabati wake.

Ametoa shauri kwa Nickolay Mladenov atakayechukua nafasi yake.

“ Tunahitaji muongozo sahihi kuhusu mwelekeo wa haya yote lakini inapaswa kuanza na pande husika, jamii ya kimataifa inaweza tu kusaidia lakini pande husika zinapaswa kuanza”