Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wenye ulemavu wapambana na maisha Afrika ya Mashariki

Watu wenye ulemavu wapambana na maisha Afrika ya Mashariki

Kamati kuhusu haki za watu wenye ulemavu mjini Geneva likikutana kuanzia Machi tarehe 25 hadi April 17, jarida maalum la Aprili, tarehe 3, linaangazia suala hilo katika ukanda wa Afrika Mashariki. 

Mkataba kuhusu haki za watu wenye ulemavu umepitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Matiafa mwaka 2006, ukiwa na lengo la kuhamasisha jamii kuhusu haki hizo pamoja na kuzitunza na kuhakikisha watu wote wenye ulemavu wanaweza kushirikishwa na jamii bila kubaguliwa. Tayari nchi 159 zimeridhia mkataba huo, zikiwemo Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi.

Lakini bado changamoto nyingi zinawakumba watu wenye ulemavu. 

Je hali ikoje katika ukanda wa Afrika ya Mashariki? Benson Mwakalinga kutoka Redio washirika Kyela FM, nchini Tanzania na John Kibego kutoka Uganda wamekutana na watu wenye ulemavu. Ungana na Joshua Mmali katika jarida hili maalum.