Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Harakati za kukabiliana na kifua kikuu nchini Kenya

Harakati za kukabiliana na kifua kikuu nchini Kenya

Mwaka huu wa 2015 shirika la afya duniani, WHO limetoa matumaini kuhusu ugonjwa wa Kifua Kikuu likieleza  kuwa hatua zimepigwa katika kudhibiti ugonjwa huo unaosababisha vifo miongoni mwa wakazi wa dunia hii. Mathalani mwaka 2013 watu Milioni Tisa waliugua kifua kikuu huku Milioni 1.5 kati yao wakifariki dunia.

Ni kwa mantiki hiyo WHO inatoa wito wa uwajibikaji na juhudi zaidi katika vita dhidi ya kifua kikuu ambao ni ugonjwa wa kuambukiza unaoua zaidi.

Hatua hizo ni pamoja na zile zilizoridhiwa na serikali kwenye mkutano wa afya wa WHO kwa kukubaliana miaka ishirini ya kumaliza janga la ugonjwa wa kifua kikuu.

Mkakati huo umeainisha hatua za serikali na wadau ili kutoa huduma kwa wagonjwa, kuwekea sera na mifumo ya kuwezesha tahadhari na huduma aidha kuhimiza utafiti ili kumaliza na kutokomeza janga la kifua kikuu.

Je nchini Kenya hali ukoje? Basi ungana na Geoffrey Onditi kutoka radio washirika ya Shirika la Utangazaji nchini Kenya KBC kupata hali halisi.