Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuyoyoma kwa visa vipvya vya Ebola kwaleta nuru kwa watoto Sierra Leone

Kuyoyoma kwa visa vipvya vya Ebola kwaleta nuru kwa watoto Sierra Leone

Sierra Leone, ni moja ya nchi tatu za Afrika Magharibi zilizokumbwa zaidi na mlipuko wa Ebola.Takwimu za hivi karibuni zaidi zinaonyesha kupungua siyo tu kwa idadi ya vifo bali pia maambukizi mapya.

Mathalani kwa wiki inayoishia tarehe 29 mwezi uliopita, kulikuwepo na visa vipya 82 vya Ebola huko Sierra Leone na Guinea ambapo Sierra Leone vimepungua kutoka asilimia 84 wiki iliyotangulia hadi asilimia 67 wiki hiyo ya tarehe 29 Machi.

Kupungua kwa visa vya Ebola kumewezesha hata vituo vya afya sasa kuanza tena kutoa huduma muhimu kama vile chanjo kwa watoto.

Kufahamu zaidi kuhusu kuanza kwa huduma hizo ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii.