Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon alaani mashambulizi ya kigaidi Kenya

Ban Ki-moon alaani mashambulizi ya kigaidi Kenya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea leo asubuhi kwenye chuo kikuu cha Garissa, nchini Kenya.

Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Bwana Ban amenukuliwa akisema anatumai hali itadhibitiwa haraka bila mateso mengine dhidi ya wale ambao bado wametekwa nyara.

Ripoti za waandishi wa habari zinasema kwamba watu angalau 70 wameuawa katika mashambulizi hayo na wengine 79 wamejeruhiwa, huku wanafunzi wengi zaidi bado wakiwa wametekwa nyara ndani ya chuo.

Katibu Mkuu amepeleka rambirambi zake kwa familia za wahanga akiwatakia nafuu waliojeruhiwa.

Aidha amekariri mshikamano wa Umoja wa Mataifa na raia na serikali ya Kenya, na jitihada zake katika kupambana na ugaidi na msimamo mkali.