Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhuru wa kusafiri wahitajika kwa msimu wa kilimo Sudan Kusini

Uhuru wa kusafiri wahitajika kwa msimu wa kilimo Sudan Kusini

Wakati msimu wa kupanda mbegu unaanza nchini Sudan Kusini, Mratibu wa misaada ya kibindamu wa Umoja wa Mataifa Tobi Lanzer ameelezea wasiwasi wake kuhusu vizuizi kwa usafiri wa raia, mapigano yanapoendelea.

Bwana Lanzer amesema vizuizi hivyo vinazuia watu kufika mashambani, kupanda mbegu, kuchunga mifugo yao na kufanya biashara.

Ameongeza kwamba uhuru wa kusafiri unahitajika ili kuzuia hali ya usalama wa chakula izorote zaidi, tayari watu milioni 2.5 wakiwa wamekumbwa na ukosefu wa usalama wa chakula, hasa katika majimbo ya Jonglei, Unity na Upper Nile, akionya kwamba idadi hiyo inaweza kuongezeka wakati wa msimu wa mwambo, ambao karibu unaanza na kuendelea hadi mwezi Agosti.

Aidha Bwana Lanzer amesema mazingira salama ni muhimu kwa mashirika ya kibinadamu kuweza kufikishia watu zaidi misaada ili kupunguza njaa na kuwawezesha watu wajitegemee.