Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yataka maeneo ya urithi yalindwe Syria

UNESCO yataka maeneo ya urithi yalindwe Syria

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO) limesisitiza wito wa kulindwa kwa urithi wa kipekee chini Syria kwa kuzingatia machafuko yanayoendelea.

Katika taarifa ya shirika hilo inayomkariri mkuu wa shirika hilo Irina Bokova, UNESCO imesema urithi wa Syria ni wa Wasyria na wanadamu wote na kutoa wito kwa pande kinzani kujizuia kutumia maeneo ya urithi wa utamaduni kwa matumizi ya kijeshi na kuvilinda kinyume na uharibifu utokanao na mapigano.

Bi Bokova ametaka pande zote kuhakikisha wanalinda eneo la urithi wa dunia la Bosra, Idlib, Maarrat al Numaan na makumbusho ya Bosra . Pia ameelezea kuridhishwa kwake kwa hatua ya hivi karibuni ambapo pande kinzani zilikubali kuondoa wapiganaji katika eneo la urithi wa dunia la Bosra.