Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yajiandaa kwa kimbuga Maysak kinachokaribia Ufilipino

UNICEF yajiandaa kwa kimbuga Maysak kinachokaribia Ufilipino

Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF, limesema kuwa limeandaa bidhaa muhimu za misaada, na kuwaweka wahudumu wake tayari kwa kutoa usaidizi wa kibinadamu, wakati taifa la Ufilipino linapojiandaa kwa kimbunga Maysak, au Chedeng kinavyoitwa na wenyeji.

Kimbunga hicho kinatarajiwa kuwasili kwenye eneo la Bicol, mashariki mwa nchi katika siku chache zijazo.

Mwakilishi wa UNICEF nchini Ufilipino, Lotta Sylwander amesema kuwa shirika hilo li tayari kuisaidia serikali ya Ufilipino kwa misaada ambayo tayari imewekwa katika maghala yake Manila, Tacloban, na Cotabato mara tu hali ya dharura itakapoanza, akiongesza kwamba la kipaumbele kwao ni kuhakikisha kuwa watoto na haki zao na maslahi yao yanalindwa kabla, wakati wa na baada ya majanga.