Kilimo kizalishe ajira zaidi:Kabaka
Mkutano kuhusu mikakati mipya ili kufikia maendeleo endelevu pamoja na kutokomeza ukosefu wa ajira umemelizika mjini New York ambapo fursa za ajira kupitia kilimo hususani barani Afrika ni miongoni mwa yaliyojitokeza.
Mkutano huo ulioandaliwa na Baraza la Uchumi na la Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC na Shirika la Kazi Duniani ILO ulijadili namna killimo kinavyoweza kusaidia asilimia 80 ya wakazi wanaoishi vijijini barani Afrika kama anayoeleza waziri wa Kazi na ajira wa Tanzania, Gaudensia Kabaka
(SAUTI KABAKA)