Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vimbunga vya Pasifiki vyaashiria tishio la mabadiliko ya tabianchi- UM

Vimbunga vya Pasifiki vyaashiria tishio la mabadiliko ya tabianchi- UM

Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kupunguza hatari za majanga, Margareta Wahlström, ameelezea wasiwasi wake kuhusu mustakhbali wa nchi za visiwa vidogo zinazoendelea, wakati zikikabiliwa na majanga ya hali ya hewa ya mara kwa mara. Taarifa kamili na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla)

Bi. Wahlström amesema ni ajabu kwamba katika kipindi cha wiki mbili tangu mkutano wa kimataifa Sendai kuhusu kupunguza hatari za majanga, mataifa ya Vanuatu na Micronesia yamelazimika kutangaza hali ya hatari kufuatia vimbunga vya daraja ya 5, ambavyo vimewaua watu kadhaa, kuwalazimu wengi kuhama, na kusababisha uharibifu mkubwa.

Mwishoni mwa wiki hii, mamilioni ya watu nchini Ufilipino huenda wakaathiriwa na kimbunga Maysak, kulingana na ukubwa wake kitakapowasili.