Ujumbe wa Tanzania UM wapata makazi ya kudumu

Ujumbe wa Tanzania UM wapata makazi ya kudumu

Ujumbe wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani umezindua rasmi jengo lake jipya lenye gorofa sita ambalo linatumiwa na nchi hiyo katika shughuli zake za uhusiano wa kimataifa na kiuchumi.

Hili ni tukio lililowaleta watanzania wengi pamoja kama anavyosimulia Joseph Msami aliyekuwa miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo iliyoongozwa na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania.