Mkuu wa WFP ziarani Malawi

1 Aprili 2015

Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, Ertharin Cousin, amewasili nchini Malawi kwa ziara ya siku mbili. Taarifa zaidi na Joshua Mmali.

(Taarifa ya Joshua)

Ziara hiyo inafuatia mafuriko yaliyotokea Malawi mwezi Januari ambapo zaidi ya watu milioni moja wameathirika na wengine 600,000 wakihitaji misaada ya chakula.

Akiwa Malawi, Bi Cousin atatembelea mradi wa mlo wa mashuleni katika wilaya ya Mangoshi. Aidha atakutana na wakulima wadogo wadogo wanaotoa chakula kwa ajili ya mradi huo na ataenda pia katika jamii iliyoathirika na mafuriko na ambayo bado inapokea misaada ya WFP.

Halikadhalika, Mkuu wa WFP atakutana na viongozi, wafadhili na washiriki wa WFP nchini humo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter