Skip to main content

Mtalaam huru Tom Nyanduga asifu mchango wa hayati Balozi Bari Bari wa Somalia

Mtalaam huru Tom Nyanduga asifu mchango wa hayati Balozi Bari Bari wa Somalia

Kufuatia mashambulizi ya tarehe 27 mwezi huu kwenye hoteli moja katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu yaliyosababisha vifo vya raia kadhaa akiwemo mwakilishi wa kudumu wa Somalia kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa Geneva, Yusuf Mohamed Ismail Bari Bari, mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu nchini Somalia, Bahame Tom Nyanduga, ametaka kuendelezwa kwa yale aliyosimamia hayati Balozi Bari Bari ikiwemo haki za binadamu.

Katika mahojiano na Priscilla Lecomte wa idhaa hii, bwana Nyanduga ameanza kwa kukumbuka jukumu muhimu la Balozi Bari Bari katika kuendeleza haki hizo nchini Somalia na pia swala la watu wenye ulemavu wa ngozi, albino duniani kote.