Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNSMIL yakaribisha sitisho la mapigano kwenye eneo la Sidra, Libya

UNSMIL yakaribisha sitisho la mapigano kwenye eneo la Sidra, Libya

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, UNSMIL, umekaribisha sitisho la mapigano na kuondoka kwa majeshi kwenye eneo la lenye mafuta la Sidra nchini humo.

Uamuzi huo unafuatia wiki kadhaa za mazungumzo kati ya kundi la Alshuruq na kikosi cha ulinzi wa mafuta ambayo yameratibiwa na UNSMIL.

UNSMIL ikipongeza pande zote kwa utashi wao na nia njema ya kumaliza mzozo wao, inaziomba kuendelea na mazungumzo ambayo yatahusu mitambo ya machimbo ya mafuta.

Aidha UNSMIL imekariri wito wake kwa pande zote wa kusitisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na kuzingatia vita dhidi ya makundi ya kigaidi ambayo yanajaribu kupanua utawala wao nchini Libya.