Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sauti za matumaini kutokana na huduma ya maji zaangaziwa UM

Sauti za matumaini kutokana na huduma ya maji zaangaziwa UM

Mwaka 2015 ukiwa ni ukomo wa muongo maalum ulioadhimishwa na Umoja wa Mataifa kuhusu maji kwa uhai, uzinduzi wa maonyesho umefanyika wiki hii kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York.

Maonyesho hayo yaitwayo Sauti za maji kwa uhai ni picha zinazoonyesha jinsi upatikanaji wa maji unavyobadilisha maisha ya watu.

Aidha uzinduzi huo umekuwa pia fursa ya kutoa tuzo ya mashindano kuhudu mada hiyo ya maji kwa uhai, yakimulika miradi bora inayolenga kuimarisha matumizi ya maji kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Joseph Msami amehudhuria tukio hilo. Ungana naye katika makala hii.