Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yapambana na ugonjwa unaothiri kondoo na mbuzi

FAO yapambana na ugonjwa unaothiri kondoo na mbuzi

Shirika la Chakula na Kilimo duniani, FAO limezindua leo kampeni ya kutokomeza tauni ya kondoo na mbuzi ifikapo mwaka 2030.

Katika taarifa iliyotolewa wakati wa mkutano maalum wa siku tatu kuhusu ugonjwa huo ulioanza mjini Abidjan, nchini Côte d’Ivoire, FAO imesema ugonjwa huo umeongezeka sana katika kipindi cha miaka 15 iliyopita na hivyo kuathiri mifugo katika nchi 70 za Afrika, Asia na Mashariki ya Kati.

Hata hivyo, FAO imeeleza kwamba chanjo ipo, kwa hiyo inawezekana kutokomeza ugonjwa huo, wala usipotibiwa, unaweza kuua asilimia 90 ya mifugo.

Daktari Juan Lubroth ni Ofisa Mkuu wa waganga wa wanyama katika shirika la FAO akizingatia umuhimu wa mifugo midogo kama kondoo na mbuzi kwa maendeleo ya jamii na usalama wa chakula.

(Sauti ya Lubroth)

Kondoo na mbuzi mara nyingi hutambulika kama ng'ombe wa watu maskini. Kwa hiyo ukiwa mkulima maskini, au kwenye jamii maskini, umuhimu wla kondoo na mbuzi ni muhimu sana na tukiweza kutokomeza kitisho hiki kwa nyama hii  inayowapatia watu lishe bora,  vitamini na protini bora vinavyochukua nafasi ya lishe itokanayo na mazao basi itakuwa ni  muhimu sana.”