Skip to main content

Umoja wa Mataifa walaani shambulizi la kambi ya wakimbizi Yemen

Umoja wa Mataifa walaani shambulizi la kambi ya wakimbizi Yemen

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Zeid Ra’ad Al-Hussein, amelaani vikali shumbulizi la angani lililofanywa Jumatatu dhidi ya kambi ya wakimbizi wa ndani ya Al-Mazraq huko Harad, kaskazini mwa Yemen, na kuzitaka pande husika katika mzozo kuwalinda raia na kuheshimu sheria ya kimataifa ya haki za binadamu na ya kibinadamu.

Cecile Pouly ni msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu

Kuna taarifa tofauti kuhusu idadi ya watu waliouawa kwenye shambulizi hilo, lakini wafanyakazi wetu nchini Yemen wamethibitisha kuuawa kwa watu wapatao 19, huku wengine wapatao 35 kujeruhiwa, wakiwemo watoto 11. Mapigano makali yameripotiwa pia katika mitaa ya mji wa Aden na kusababisha vifo.”

Bi Poully Amesema tangu Machi 27, raia wapatao 93 wameuawa, na 364 kujeruhiwa katika miji ya Sanaá, Sa'da, Dhale, Hudayda na Lahj, na kuongeza kuwa nyumba za watu binafsi, hospitali, taasisi za elimu na miundo mbinu vimeharibiwa, na mamia ya raia kukimbia makwao.