Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo wa upatikanaji wa chakula unahatarisha afya ya binadamu:WHO

Mfumo wa upatikanaji wa chakula unahatarisha afya ya binadamu:WHO

Kuelekea siku ya afya duniani tarehe Saba mwezi ujao, Shirika la afya duniani, WHO linakadiria ongezeko la maambukizi ya magonjwa kupitia vyakula kutokana na mfumo wa upatikanaji wa bidhaa hiyo kutoka inakozalishwa hadi kwa mlaji.Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Ripoti ya Assumpta)

Taarifa ya WHO kanda ya Ulaya inasema kuna mlolongo mrefu na mgumu wa upatikanaji wa vyakula hivi sasa kuliko ilivyokuwa awali hivyo ni lazima kuboresha mifumo hiyo baina ya sekta husika.

Mkutano wa kanda hiyo Dkt. Zsuzsanna Jakab ametaja miongoni mwa sababu kuwa ni utandawazi, kubadilika kwa mienendo ya ulaji, teknolojia mpya, mabadiliko ya tabianchi.

Dkt. Jakab amesema ni vyema kuanza kuwa makini wakati huu ambapo dunia inasahau kuwa watu wanaweza kuathiriwa na kemikali na vimelea vilivyomo kwenye vyakula kama vile Salmonella.

Amesema ukosefu wa umakini kwenye mlolongo mzima kuanzia mazingira ya uaandaji, uzalishaji, mapishi na hata uhifadhi yanaweza kuwa na athari za kiafya na kiuchumi wakati huu ambapo watu wanaweza kupata vyakula hata wakati ambao sio msimu wake.