Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amezikwa na Boko Haram angali mzima: Ibrahim, miaka 10

Amezikwa na Boko Haram angali mzima: Ibrahim, miaka 10

Kwa kipindi cha miezi kadhaa iliyopita, kaskazini mwa Cameroon, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR limekuwa likipokea maelfu ya raia wa Nigeria wakikimbia mashambulizi ya kundi la kigaidi la Boko Haram.

Baada ya kuwapokea mpakani, wengi wakiwa wamejeruhiwa, kubakwa au kuathiriwa na njaa, UNHCR linawapa hifadhi wakimbizi hao kwenye kambi ya Minawao iliyoko kilomita 90 kutoka mji mkuu wa jimbo la kaskazini, na tayari likitarajia kufungua kambi nyingine.

Kwenye kambi ya Minawao, wakimbizi wanajaribu kuendelea na maisha, wengine bado wakiathirika na majeraha yao. Mmoja wao ni Ibrahim, mvulana wa miaka 10. Ungana na Priscilla Lecomte akikuhadithia aliyoyapitia.