Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya kibinadamu Syria inazorota kila siku- Valerie Amos

Hali ya kibinadamu Syria inazorota kila siku- Valerie Amos

Suluhu la kisiasa linapaswa kupatikana haraka nchini Syria, kwani hali ya kibinadamu inazidi kuzorota kila uchao. Hayo yamesemwa na Mratibu Mkuu wa Masuala ya Kibinadamu, Valerie Amos, wakati akihutubia mkutano wa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotoa ufadhili kwa watu wa Syria katika mji mkuu wa Kuwait, Kuwait.

Bi Amos amesema watoto ndio walioathiriwa zaidi, watoto milioni 5.6 wakihitaji usaidizi, huku zaidi ya milioni 2 wakiwa hawaendi shule, kwani robo ya shule za Syria zimeharibiwa au kugeuzwa makazi ya wakimbizi.

Amesema wakati Kuwait ikiwa mwenyeji wa mkutano wa tatu wa kuahidi misaada kwa Syria, wito wa Umoja wa Mataifa na wadau wake mwaka huu ni kwamba, iwasaidie raia wa Syria ndani ya nchi, walio ukimbizini na jamii za wenyeji wao katika nchi jirani, pamoja na serikali za nchi jirani ambazo zitahitajika kupanua huduma zao katika sekta za afya na elimu.

Mkutano wa Kuwait utafunguliwa hapo kesho na Amir wa Kuwait, Sheikh Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah, na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mr. Ban Ki-moon. Bi Amos amesema bila mikutano hiyo ya ahadi za ufadhili ambayo imesaidia kuchangisha mabilioni ya fedha, watu wengi zaidi ndani na nje ya Syria wangekuwa wanahaha kuishi