Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Moustapha Soumaré awasili Sudan Kusini kama Naibu Mkuu wa UNMISS

Moustapha Soumaré awasili Sudan Kusini kama Naibu Mkuu wa UNMISS

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, umetangaza kuwasili kwa Bwana Moustapha Soumaré, akiwa ni Naibu Mwakilishi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya kisiasa nchini humo.

Taarifa ya UNMISS imesema Bwana Soumaré anauchukua wadhfa huo akiwa na uzoefu mkubwa katika operesheni za ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa, masuala ya kibinadamu na maendeleo.

Kabla ya kujiunga na UNMISS, Bwana Soumaré alikuwa Naibu Mwakilishi wa Katibu Mkuu katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC, MONUSCO, tangu Oktoba mwaka 2012, ambako alishikilia pia wadhfa wa Mratibu Mkaazi wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo, UNDP.

Aliwahi kuhudumu pia katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Liberia, UNMIL, na Mratibu na Mwakilishi Mkaazi Benin na Rwanda. Mnamo mwaka 2007, aliteuliwa kuwa Naibu Msimamizi wa UNDP na Naibu Mkurugenzi wa Ofisi ya Ukanda wa Afrika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York.