Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajira zisizo rasmi na ukosefu wa ajira ni changamoto: rais Kikwete

Ajira zisizo rasmi na ukosefu wa ajira ni changamoto: rais Kikwete

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete leo amehutubia katika kongamano la siku tatu kuhusu mikakati mipya ili kutokomeza ukosefu wa ajira, linalofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, mjini New York.

Amesema nchi za kiafrika zimezalisha ajira milioni 37 kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita, wakati kila mwaka ni vijana milioni 122 ambao wanaingia kwenye soko la kazi, akisema hiyo ni changamoto.

Mkutano huo ambao umeandaliwa na Baraza la Uchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC na Shirika la Kazi Duniani ILO utamulika hali ya wafanyakazi wengi duniani ambao wanakumbwa na hali ngumu ya maisha, wakiwa na kazi zisizo kuwa rasmi, mishahara midogo au kazi zisizokuwa imara.

Gaudencia Kabaka ni Waziri wa Kazi na Ajira kutoka Tanzania na anaelezea matarajio ya mkutano huo kuhusiana na ajira zisizo rasmi.

(Sauti ya Waziri Kabaka)