Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yakanusha kuwepo kwa Ebola Iraq

WHO yakanusha kuwepo kwa Ebola Iraq

Shirika la Afya Ulimwenguni,WHO kwa kushirikiana na wizara ya afya ya Iraq imekanusha taarifa za kuwepo kwa kisa cha Ebola mjini Abu Gharib kusini mwa Baghdad.

Taarifa ya WHO inasema mnamo March 28 chombo kimojawapo cha habari nchini Iraq kiliripoti kuwepo kwa kisa cha Ebola nchini humo na hivyo shirika hilo likaendesha  uchunguzi ili kubaini ukweli wake.

Shirika hilo la afya ulimwenguni linasema maabara za nchini Iraq hazina uwezo wa kiufundi wa kuthibitisha kisa cha Ebola kupitia uchunguzi wa kitaalamu.