WFP yataka dunia kunusuru watu wa Syria

WFP yataka dunia kunusuru watu wa Syria

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeishukuru taifa la Kuwait kwa kusaidia katika operesheni za ugawaji vyakula nchini Syria na kutolea mwito jumuiya ya kimataifa kuendelea kusaidia jamii za watu wa nchi hiyo wanaoathiriwa na mgogoro unaondelea.Taarifa ya shirika hilo inasema kuongezeka kwa mahitaji ya dharura kunakwenda sambamba na ufinyu wa rasilimali za malighafi huku watoto wakitajwa kuathirika zaidi ambapo wameshuhudia siku 1000 katika hali ya machafuko bila kupata chakula toshelevu na lishe.

WFP inasema ni lazima kuhakikisha msaada wa chakula unalenga mahitaji ya ustawi kwa ajili ya watu walioko katika mazingira hatari kutokana na kuathiriwa na vita vinavyoingia mwaka wa tano. Katika kunusuru watoto shirika hilo la mpango wa chukula limeanisha mpango maalum wa kushirikiana na shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na wadau wengine kuhamasisha watoto kwenda shule kupitia mpango wa kutoa lishe mashuleni.