Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon aipongeza Nigeria kwa uchaguzi

Ban Ki-moon aipongeza Nigeria kwa uchaguzi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amewapongeza watu wa Nigeria kwa kufanya uchaguzi ambao ameutaja kuwa wenye amani na utulivu kwa ujumla.

Aidha amelaani mashambulizi yaliyoripotiwa kufanyika na Boko Haram na wengine ambao wamejaribu kuzorotesha utaratibu wa uchaguzi.

Uchaguzi ukiendelea leo jumapili, Katibu mkuu amewaomba wanigeria wote waendelee kukuza hali hiyo ya utulivu na kuwa na subira katika uchaguzi hadi kutangazwa kwa matokeo.

Hatimaye, Ban Ki-moon ameeleza kuamini kwamba mafanikio ya utaratibu huo yatakuwa hatua muhimu katika kuimarisha demokrasia na utawala wa sheria nchini Nigeria.