Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon atumainia uchaguzi wa Nigeria wenye amani

Ban Ki-moon atumainia uchaguzi wa Nigeria wenye amani

Leo ikiwa unafanyika uchaguzi wa rais na wabunge nchini Nigeria, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewaomba raia wote waende kupiga kura kwa wengi.

Amekaribisha azimio la pamoja lililotolewa na wagombea rais Goodluck Jonathan, na aliyekuwa rais zamani, Jenerali mstaafu Muhammadu Buhari, la kuheshimu matokeo ya uchaguzi na kutaka uchaguzi uwe wenye uwazi, usawa na utulivu.

Aidha ameipongeza Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi kwa jitihada zake katika kuandaa uchaguzi.

Akisema mafanikio ya uchaguzi yanategemea kila mdau Nigeria, awe mwanasiasa, kiongozi wa dini au jamii, jeshi, raia, Ban Ki-moon amewasihi wagombea na wafuasi wao kutatua mvutano unaoweza kuibuka baada ya uchaguzi kwa njia ya amani.