Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulinzi wa amani uzingatie eneo husika: Jenerali Mwamunyange

Ulinzi wa amani uzingatie eneo husika: Jenerali Mwamunyange

Wakuu wa majeshi ya ulinzi na usalama kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wanakutana jijini New York kwenye kikao cha siku moja. Lengo ni kujadili mustakhbali wa shughuli za ulinzi wa amani za Umoja huo wakati huu ambapo changamoto mpya zinaibuka. Umoja wa Mataifa unasema miongoni mwa changamoto hizo ni kutakiwa kulinda amani sehemu ambazo hakuna amani. Je nini matarajio ya Tanzania ambayo nayo imetuma askari wake kulinda amani katika nchi mbali mbali ikiwemo Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC na Lebanon? Mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini Tanzania Jenerali Davis Mwamunyage ameeleza kwa muhtasari katika mahojiano yake na Assumpta Massoi wa Idhaa hii kabla ya kuanza kwa kikao hicho.