Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhaba wa Maji na harakati za kusaka raslimali hii adhimu

Uhaba wa Maji na harakati za kusaka raslimali hii adhimu

Maji ni uhai, huu ni usemi maarufu sana miongoni mwa wengi lakini usemi hauonekani kutimia kwa nchi nyingi zinazoendelea kutokana na ukosefu wa rasilimali hii adhimu.Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo ya Maji iliyozinduliwa mwezi huu huko India, ifikapo mwaka 2030 uhaba wa maji duniani utakuwa pungufu kwa asilimia 40 iwapo hatua za dhati hazitachukuliwa kusimamia rasilimali hiyo.

Ripoti hiyo na nyinginezo tangulizi zinasema hilo liko dhahiri kutokana na uhusiano wake na mabadiliko ya tabianchi.

Kama hiyo haitoshi inasema hatua hizo ni lazima kwa kuwa kufanikiwa maendeleo endelevu kuna uhusiano mkubwa na uwepo wa maji na huduma za kujisafi. Hivyo ni changamoto kubwa kwani maji ni suala mtambuka kote duniani. Bara la Afrika linaangaziwa kwa kukabiliwa na uhaba huo ambao ripoti za hivi karibuni zimetaja nchi kama vile Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo DRC,na Msumbiji kuwa vinara wa ukosefu wa maji jambo linalopeleka madhila kwa nusu raia wa nchi hizo.

Nchini Tanzania hali ikoje? Tuungane na Pili Mlindwa wa redio washirika Pangani Fm ya Tanga anayeangazia uhaba wa maji nchini humo.