Skip to main content

WHO yahitaji dola 124 kutoa misaada ya kiafya Syria

WHO yahitaji dola 124 kutoa misaada ya kiafya Syria

Mgogoro wa Syria ukiwa unaingia mwaka wa tano na ikiwa ni siku chache kabla ya kongamano la tatu la kimataifa la changizo la kibinadamu, shirika la afya ulimwenguni WHO linataka kiasi cha dola 124 ili kuendelea na usaidizi wa kiafaya katika Jamhuri ya Kiarabu ya Syria.

Akiongea mjini Geneva mwakilishi wa WHO mjini Damascus Dk Elizabeth Off  amesema hali ya kibinadmau ni mbaya nchini humo na msaada wa dhrura unahitajika husuani mjini Allepo

(SAUTI ELIZABETH)

"Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni moja na laki tatu wanahitaji msaada ya kitabibu mjini Allepo wakati huu ambapo idadi kubwa ya hospitali zimeharibiwa."

Amesema nchi nzima inahitaji misaada ya kiafya kufuatia mapigano yanayoendelea katika majimbo mbalimbali.