Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wa WFP wafikia watu 160,000 Vanuatu

Msaada wa WFP wafikia watu 160,000 Vanuatu

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP limesema leo kwamba tayari vyakula vya msaada vimefika kwenye visiwa 22 ambavyo vimeathirika na kimbunga PAM, nchini Vanuatu.

Taarifa ya WFP imesema kwa sasa wanasaidia harakati zianzoongozwa na serikali za kupanga masuala ya mgao wa misaada, huduma za vifaa na usafirishaji na kuwapatia vyakula vya ziada pale vile vinavyotolewa na serikali unapopwaya.

Biskuti zenye vitamini zimepelekwa kwenye maeneo ambapo watu hawajarudishiwa huduma za maji na umeme na hivyo hawawezi kupika ambapo WFP inasema itahitaji dola Milioni Sita kwa ajili ya misaada ya chakula na dola zaidi ya Milioni Mbili kwa shughuli za vifaa, usafirishaji na mawasiliano.

Tayari Umoja wa Mataifa ulishatoa ombi la takribani dola Milioni 30 kwa ajili ya usaidizi wa watu 166,000 nchini Vanuatu kwa miezi mitatu.

Tayari Umoja wa Mataifa ulishatoa ombi la takribani dola Milioni 30 kwa ajili ya usaidizi wa Vanuatu watu 166,000 nchini Vanuatu kwa miezi mitatu.