Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhalifu wa jinai Mashariki ya Kati ukabiliwe kwa dharura- Ban

Uhalifu wa jinai Mashariki ya Kati ukabiliwe kwa dharura- Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema leo kuwa makosa ya jinai yanayofanywa katika ukanda wa Mashariki ya Kati yanahitaji kukabiliwa kwa dharura. Ban amesema hayo wakati akilihutubia Baraza la Usalama, ambalo limekutana leo kufanya mjadala wa wazi kuhusu wahanga wa mashambulizi na ukiukwaji dhidi ya makundi ya walio wachache kikabila au kidini Mashariki ya Kati.

Katibu Mkuu amesema, ni lazima kutowawajibisha wanaotenda makosa ya jinai dhidi ya jamii yoyote au jamii zote kukome.

“Nasisitiza pia kuwa ukiukwaji unaotekelezwa wakati wa kupambana na ugaidi unakwenda kinyume na maadili, na hauwezi kuleta ufanisi. Utendaji wa uhalifu hauwezi kamwe kuziondolea serikali jukumu lao la kutimiza wajibu wao wa kulinda haki za binadamu.”

Ban amesema washauri wake kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari na wajibu wa kulinda raia, walionya Agosti mwaka uliopita kuwa vitendo vya kundi la Daesh viliashiria utekelezaji wa mauaji ya kimbari.

“Kuna ushahidi wa dhati kuwa wanajamii kadhaa za walio wachache wamekuwa wahanga wa uhalifu dhidi ya ubinadamu, uhalifu wa kivita na ukiukwaji mwingine mbaya wa haki za binadamu. Walioathirika hasa ni wanawake na wasichana.”

Akizungumza kuhusu Syria, Ban amesema mzozo nchini humo unapoingia mwaka wa tano, kutoawawajibisha wanaokiuka haki za binadamu kumesababisha kuongezeka kwa uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu na ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu, ukifanywa na pande zote, mathalani vikosi vya serikali na makundi yenye silaha, hususan Daesh na

Jabhat al Nusra.