Ban afungua mkutano wa wakuu wa majeshi ya ulinzi duniani
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amefungua mkutano wa kwanza kabisa wa wakuu wa majeshi ya ulinzi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa akitaja mambo mawili ambayo ni muhimu kuimarisha operesheni za ulinzi wa amani za umoja huo.
Mosi mchango wa askari na vifaa pindi ujumbe unapoanzishwa na pili utashi wa kisiasa kwa kuwa..
(Sauti ya Ban)
“Iwapo tutasaidia nchi hizo kupatia ulinzi raia wake na uongozi shirikishi, tunaweza kutatua machungu ambayo yanachochea mbegu ya misimamo mikali na kueneza mitandao ya kigaidi duniani.”
Tanzania katika mkutano huo inawakilishwa na Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Jenerali Davis Mwamunyange ambaye ameeleza mambo ya kuzingatiwa.
(Sauti ya Jenerali Mwamunyange)